Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kupitia Umoja wa Wabunge Wanawake wakiendesha Semina ya siku mbili kwa Wabunge vinara wa masuala ya Jinsia (Gender Champions), kuhusu Bajeti yenye Mrengo wa Kijinsia ili kuwawezesha wabunge hao kuwa na mtazamo wa kijinsia katika upangaji na Utekelezaji wa Bajeti ya serikali na sekta mbalimbali. Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), pia ilitumia fursa hiyo kuendelea kuwajengea uwezo Wabunge hao juu ya Haki za Wanawake za Ardhi na Uthabiti wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa.
#BajetiJumuishi
#BajetiYenyeMrengowaKijinsia

