TGNP Publications
KUFANYA MABADILIKO: Vibonzo
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirkiana na shirika la kimataifa la watu wa Canada (GAC) kupitia shirika la SeedChange lililopo nchini Canada, tunatekeleza mradi wa pamoja ujulikanano kama “Wanawake wa Vijijini Waleta Mabadiliko—Rural Women Cultivating Change (RWCC)”.
Kitabu hiki cha katuni au maarufu kama Vibonzo kimetengenezwa kutoa njia rafiki kwa watu kutafakari, kufikiri, na kujadili baadhi ya masuala muhimu katika jamii ya Tanzania. Kupitia mchakato wa ushirikishwaji, waaandaaji wa kitabu hiki walitaka kuonesha, kwa kutumia katuni na hadithi rahisi, uhusiano kati ya unyanyasaji wa kijinsia, kilimo cha ikolojia, na ushiriki wa wanawake katika uongozi na maamuzi. Tunatumaini kuwa kwa kusoma kitabu hiki pamoja, wanajamii, hasa vijana wa vijijini, watajifunza njia ya kupaza sauti zao na kuwa vinara wa kuleta mabadiliko.
Wanafanya maamuzi pia wanaweza kujifunza mengi kuhusu kilimo cha ikolojia na njia zinazoweza kusaidia kilimo kama njia ya kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili wakulima, wanawake vijana, watu wanaoishi na ulemavu, na makundi mengine yaliiyopembezoni katika maeneo ya vijijini–-na kusaidia kuwawezesha kiuchumi.
MWONGOZO WA KUJIFUNZA KUPIMA MABADILIKO KATIKA VIBONZO
Mwongozo huu utakusaidia namna ya kutumia maudhui haya kwa njia sahihi, ili kuwezesha uelewa katika jamii na pia kuweza kuchukua hatua juu ya vitu ulivyojifunza.
Unaweza tumia mwongozo huu kwa tengeneza majukwaa ya mijadala ya vikundi kwa ajili ya usomaji au usikilizaji kuwashirikisha
wanakikundi.
Pakua mwongozo wa kujifunza kwa vitendo kwa kitabu hiki cha katuni kwa Kiswahili:
SAUTI NA VIDEO YA KITABU CHA KUFANYA MABADILIKO: VIBONZO
Katika wasilisho hili, utatusikia tukielezea vibonzo na kuzungumza juu ya kile tunachokiona, na kusoma kwenye kitabu. Unaweza kusikiliza, kutazama, au kufuata kwa muda mrefu na kitabu kilichochapishwa, ukiwa peke yako au Pamoja na wengine katika kikundi. Unaweza kusimamisha video wakati wowote ili kuzungumza kuhusu ulichosikia na kuona kisha uendelee ukiwa tayari.