Wafanyabiashara wa sokoni wametakiwa kuendele kutumia njia za asili za kusindika mboga na matunda ili kuondokana na hasara zisizo za lazima kwa kutupa bidha hizo zinaponyauka au kuoza.
Hayo yameelezwa jana Julai 23 na Makamu Mwenyekiti wa kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Saranga Maria Mwigune, wakati kituo hicho kikitoa elimu kwa wajasiriamali wa Soko dogo la Kimara Temboni juu ya usindikaji wa mboga na matunda.
Aidha Makamu Mwenyekiti huyo amesema kuwa wao kama kituo wameamua kuwafundisha wajasiriamali hao baada ya wao kupewa elimu hiyo na shirika lisilo la kiserikali ambalo ni TGNP, Na hii ikiwa ni sehemu ya mrejesho wao wa mafunzo waliyopewa julai 15 mwaka huu.
Ameongeza kuwa mbinu hizo walizowapa za kusindika zitawasaidia wafanyabiashara hao kwani mboga na matunda uweza kukaa kwa muda mrefu Zaidi bila kuharibika na wataweza kuepukana na hasara za mara kwa mara za kutupa mboga, Na kuongeza kuwa njia hiyo inatumiwa pia na maduka makubwa (supermarket) ya ndani na nje ya nchi.
Amesisitiza kuwa licha kutoa elimu ya ujasiriamali lakini pia wametoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa kwani maeneo ya sokoni vitendo hivi vinakuwa vingi hasa rushwa za ngono na ukatili wa kiuchumi, Na kuwafundisha endapo tukio hilo litatokea nini wafanye au wakatoe ripoti wapi.
Na mwisho ameongeza kuwa amefurahishwa na muitikio wa washiriki kwani wamepata watu Zaidi ya 100 na hasa wababa wamejitokeza kwa wingi sana, Hii inaleta picha nzuri kwa kuona vitendo hivi vya ukatili tunakwenda kuvitokomeza na kuvisambaratisha kabisa.
Kwa upende wake Mwenyekiti wa soko hilo la Temboni Bi. Erineka Lyimo amesema kuwa elimu hiyo waliyopata itawasaidia watu wake kwa Nyanja zote kwani mambo yakutupa tena mboga wala matunda hayatakuwepo, lakini pia vitendo vya ukatili vitapungua kuanzia hapo sokoni mpaka majumbani kwani hata wababa wamejua pa kupeleka malalamiko yao endapo watanyanyaswa na wenza wao.
Ameendelea kusema kuwa amefurahishwa pia na somo la bidhaa za urembo wa asili(culture) kama hereni na Vidani kwani wanawake wengi watapunguza muda ya kupiga umbea na badala yake watafanya kazi ya kutengeneza hivyo vitu ili kujiongezea kipato chao.
Na mwisho ametoa wito kwa wanaume wasione aibu kuwasilisha malalamiko yao endapo watafanyiwa ukatili wa aina yoyote na kutoa ahadi ya kuwa wao kama wajasiriamali wadogo watazidi kuisambaza elimu hiyo mbali Zaidi ili jamii iweze kunufaika na elimu hiyo.