LUCIA Akaro, mwakilishi wa EKAMA Development Foundation Tanzania amesema kuna haja ya mifumo kandamizi kwa wanawake kukemewa .
Akaro ametoa kauli hiyo wakati akiwasilisha mada ya ardhi,kilimo, uzinduaji,uchimbaji madini na mabadiliko ya tabia nchini kwa wanawake na makundi yaliyoko pembezoni wakati wa warsha zinazoendelea katika tamasha la jinsia la 14 liloloandaliwa na mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP – Mtandao )
“Kundi la wanawake ndilo kundi linaloathirika zaidi na mabadiliko ya Tabia nchi Katika kupambana na ukatili wa kijinsia. Kuna haja ya kuanzisha majukwaa mbali mbali ya utoaji wa elimu kwa jamii ili kuondokana na unyanyasaji wa familia kupitia ardhi ama mavuno “

Dada Akaro akiendesha warsha katika viwanja vya TGNP Mtandao kwenye TAMASHA LA JINSIA 2017.
Alizitaja athari zitokanazo na ukatili wa jinsia kuwa ni kupungua kwa nguvu kazi pamoja na kipato cha wanawake kinachopelekea kuwepo kwa umaskini ,kupungua kwa uhifadhi wa chakula na kukosekana kwa muda wa kutosha kufanya kazi shambani kutokana na vitendo vya kikatili .
Katika kutatua changamoto hizo amesema katika sekta ya kilimo kuna haja ya kuwajumuisha wanawake katika mnyororo wa thamani wa kilimo ili kungeza bei ya mazao na kuteneneza nafasi nyingi za ajira . kuongeza jitiada katika kuzuia upotevu wa mazao kipindi cha uvunaji na baada ya uvunaji kwa kuhifadhi mazao vizuri katika maghala au katika mapipa maalum na Serikali iongeze bajeti yenye mlengo wa kijinsia katika sekta ya kilimo.
“Ni muhimu kujumuisha masuala ya mabadiliko ya Tabia nchi katika mipango na bajeti kuanzia ngazi ya serikali za mitaa hadi ngazi ya taifa. Elimu itolewe kwa jamii kuhusu athari za ukatili wa jinsia, Wanaume wahusishwe katika mapambano ya kupinga ukatili wa jinsia,” amesema Akaro.
Aidha, Nembris Mollel mshirikmi wa warsha hiyo amesema “asasi zinazoshughulika na harakati za kumkomboa mwanamke kuiga mfano wa TGNP Mtandao kwa kuwatembelea wananchi wa pembezoni badala ya kujikita mijini pekee.”