+255 (754) 784-050

Call us

Mabibo, Dar es salaam

Ubungo

Tamasha la Jinsia Taarifa kwa Vyombo vya Habari

TGNP MTANDAO

TAMASHA LA JINSIA 2015

1-4 September 2014

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 MADA KUU

‘Jinsia, Demokrasia na Maendeleo: Mageuzi ya Mifumo Kandamizi Hayaepukiki’

 

Tamasha la Jinsia 2015

Tamasha la Jinsia ni jukwaa la wazi linaloleta pamoja wanaharakati , watu binafsi, vikundi  na mashirika kutoka ngazi mbalimbali Tanzania na nje ya Tanzania kubadilishana uzoefu, kujengeana uwezo na kutafakari na kusherehekea changamoto na mafaniko  katika kufikia usawa wa kijinsia . Hili ni tamsha la Jinsia la 12 tangu kuanzishwa kwake mara ya kwanza mwaka 1996.  Waandaji wamefanikiwa kuwa na ongezeko la washiriki kutoka 400 ( mwaka 1996) hadi  zaidi ya 5000 (mwaka 2011 na 2013). Kukua kwa matamsha haya kulileta hitaji la kuwa na matamasha ya ngazi ya jamii tangia mwaka 2010 huko Mkambarani Morogoro hadi 2014 huko Tarime Mara.

Kuhusu Mada kuu                            

Mada kuu ya Tamahsa la Jinsia mwaka 2015 ni ‘Jinsia, Demokrasia na Maendeleo: Mageuzi ya  Mifumo Kandamizi Hayaepukiki’. Uwepo na kuendelea kwa ukisefu wa usawa wa kijinsia unatokana na sababu mbalimbali ikiwemo mifumo kandamizi iliyojengeka katika jamii ikiwa imejifunganisha na mfumo dume unaowaweka pembene wanawake kama kwamba wao si sehemu muhimu katika jamii yetu.

Mifumo kandamizi ipo katika nyanja zote za maisha ikiwa ni pamoja na mifumo kandamizi ya kiuchumi (inayomnyima mwanamke haki stahiki za kiuchumi, kumiliki na kunufaika na rasilimali kama sehemu ya jamii). Kuendelea kukua na kupanuka kwa pengo kati ya wenye nacho na wasiokuwa nacho, matajiri na masikini kunaendeleza mgawanyiko usio sawa wa rasilimali huku wachache wakimiliki kiasi kikubwa cha rasilimali. Katika mazingira hayo ni vigumu kufikia usawa wa kijinsia. Vilevile mifumo kandamizi ya kijamii ambayo mingi imejikita katika tamaduni kandamizi zinazokosa jicho la kinjsia hivyo kuendeleza ukatili wa kijinsia na mambo mengine kadha wa kadha.

Aidha mifumo kandamizi ya kisiasa inayomnyima mwanamke haki ya uongozi na ushiriki katika shuguli za kidemokrasia imeendelea kukithiri huku idadi ndogo ya wanawake ikiwa na nafasi za uongozi kuanzaia serikali za mitaa hadi serikali kuu, bunge, mahakama na nyadhifa nyingine tofauti tofauti. Suala hili litaangaliwa kwa mapana yake katika warsha ya masuala ya uchaguzi na katiba itakayofanyika wakati wa tamasha. Kwa ujumla ipo mifumo mingi kandamizi kwa mwanamke na makundi mengine muhimu ambayo inaendelea kufifisha maendeleo ya makundi haya kwa muda mrefu.

Licha ya uhuru kwa muda wa miaka zaidi ya hamsini bado mifumo ya elimu, afya, maji, umeme na huduma nyinginezo si rafiki kwa makundi hayo hivyo kuhitaji mageuzi makubwa. Mageuzi makubwa ya mifumo kandamizi ya kisiasa, kijamii, kiuchumi na kiutamaduni ni muhimu katika nchi yetu na hivyo basi ili kufikia usawawa wa kijinsia, demokrasia shirikishi na kweli na maendeleo endelevu, ni dhahiri kuwa mabadiliko ya mifumo hiyo hayaepukiki.

Waandaaji

Tamasha la Jinsia linaandaliwa na TGNP Mtandao kwa kushirikiana na wanaharakati watetezi wa masuala ya Jinsia na haki za Binadamu ( FemAct), jukwaa la wanawake na Katiba, pamoja na mashirika na taasisi nyingine zenye mrengo unaofanana. Pia Tamsha hili linaandaliwa kwa kushirkiana na wanajamii kutoka Semina za Jinsia na Maendeleo ( GDSS) kutoka TGNP Mtandao, wanaharakati wa ngazi ya jamii kutoka katika vituo vya taarifa na maarifa ambao ni wadau muhimu katika ujenzi wa tapo la mabadailiko.

Malengo ya Tamasha la Jinsia 2015

  • Kujitathmini, kubadilishana uzoefu wa mabadiliko yanayotokea katika ngazi mbalimbali kwenye masuala ya jinsia, au mahusiano ya kitabaka, ili kuanzisha uchambuzi mpya kuhusu masuala ya jinsia, uwezeshwaji wa wanawake na mabadiliko ya kijamii katika muktadha wa kuatafuta mikakati endelevu ya maendeleo endelevu na yanayozingatia usawa, yakihusisha mashirika ya kiraia
  • Kuendeleza uelewa wa dhana ya ukombozi wa wanawake kimapinduzi kwa vitendo, ikiwa ni pamoja na kuweka kumbukumbu za harakati na mapambano mahususi dhidi ya mfumo dume na ubeberu, na namna gani ya kuboresha tapo katika ngazi zote;
  • Kusherehekea mapambano yanayofanywa na wanaharakati pamoja na mafanikio yao katika kupigania na kufanikisha mabadiliko ya kijamii katika ngazi zote za jamii;
  • Kupanua na kuboresha mitandao ya watu binafsi namashirika ya kiraia yanayofanya kazi kwa mtazamo unaofanana katika ngazi ya jamii, taifa na kimataifa ili yaongoze kushawishi kuleta maendeleo yenye usawa kwa watu wote.

Siku ya Kwanza:

Inahusisha ufunguzi waTamasha la Jinsia, uzinduzi wa Maonesho ya Jinsia na onyesho la Mahakama ya wazi. Pia siku hiyo itakuwa na tukio la uzinduzi wa ilani ya Wanawake Wapiga Kura (Women Voters Manifesto) iliyoandaliwa na mtandao wa wanawake wa katiba na uchaguzi. Ilani hiyo yenye madai na matarajio ya wanawake kwa wagombea, vyama na serikali ijayo, imeandaliwa mahsusi kabisa kwaajili ya fursa ya Uchaguzi mkuu 2015. Tunaamini kuwa, Uchaguzi mkuu 2015 ni fursa ya kuondoa mifumo kandamizi. Uzinduzi huo utafuatiwa na mjadala wa masuala ya Uchaguzi na Katiba. Siku hii italenga kushirikishana harakati mbalimbali katika kuwa na mfumo wa kidemokrasia ambao ni shirikishi, kudai haki za wanawake katika Katiba na Uchaguzi.

Siku ya Pili:

Kutakua na uwasilishaji wa mada mahsusi itakayowasilishwa na Prof. Amina Mama kutoka Nigeria ambaye ni mwanaharakati wa masuala ya kijinsia kwa muda mrefu katika maeneo mbalimbali duniani hususani katika bara la Afrika. Inahusisha jopo la watoa mada amabo watatoa mwelekeo wa mada ya siku hiyo.Siku hii italenga kubadilishana uzoefu wa mapambano wanayofanya wanaharakati na mafanikio waliyofikia.Washiriki watapata fursa yakutoa mifano dhahiri wanayo pambana  nayo kubadilisha mifumo kandamizi,mafanikio, changamoto na waliyojifunza kwenye michakato huo. Siku hii pia itafuatiwa na warsha zipatazo nane (8) zitakazokuwa na uswashilishaji wa mada mbalimbali na washiriki kutoa mawazo na maoni yao juu ya mada hizo. Mada hizo ni kama zilivyoorodheshwa.

Siku ya Tatu:                                                       

Warsha za siku ya pili na ya tatu mchana zitaandaliwa kwa namna ya kujenga uwezo na ujuzi kwenye utetezi, kujipanga kimkakati na ujenzi wa tapo.Hizi ni pamoja na warshajuu ya:, sanaa (muziki, mashairi, ngoma, namchezo wa kuigiza), ufikiwaji wa taarifa kupitia vyombo vya habari naTEHAMA, huduama za maji, afya, elimu na masuala ya uchumi na rasilimali pamoja na masuala mengine.

Siku ya nne

Siku ya nne itajikita katika kuweka mikakati ya mbeleni ambapo kila warsha itatoa na kuwashirikisha watu wengine hatua madhubuti zitakazochukuliwa baada ya Tamasha, kubainisha wadau muhimu katika utekelezaji pamoja na muda wa utekelezaji. Siku ya mwisho ya tamasha itahitimishwa kwa hotuba kutoka kwa msemaji atakayeandaliwa.

Scroll to Top