Tanzania Gender Networking Programme logo

+255 (754) 784-050

Call us

Mabibo, Dar es salaam

Ubungo

TGNP Publications

WANAWAKE WALIOSHIKA USUKANI: Simulizi za Ujasiri, Uthubutu, na Mafanikio

Kitabu hiki kimejumuisha simulizi zinazowahusu Madiwani: Emmy Rajabu Kiula, Anna Laurent Mgela, na Elizabeth James Urio. Hizi ni simulizi zenye kuakisi dhana ya uongozi shirikishi na utumishi kwa kuzingatia mahitaji ya wanyonge, wakiwamo wanawake, vijana, na watu wanaoishi na ulemavu.

Machapisho haya yanayopatikana bure na yanaambatana na mwongozo wa kujifunza ulioandaliwa kukuwezesha kutumia vizuri machapisho haya kujifunza na kuchukua hatua zitakazopelekea mabadiliko chanya.

Unaweza kupakua hapa chini vitabu kwa epdf, au video, au sauti, na pia nyimbo na maigizo.

Unaruhusiwa kuwashirikisha na wenzako. Maudhui haya yanapatikana bure kwa ajili ya kusoma, kusikiliza na kutizama.

Learning Leadership Active Learning Guide image

KUJIFUNZA KUHUSU UONGOZI: Mwongozo wa Kujifunza kwa Kushiriki

Mwongozo huu wa Kujifunza kwa Kushiriki utakusaidia kutumia maudhui haya juu ya ushiriki wa wanawake katika uongozi kwa namna itakayokuletea matunda, na kuwezesha uelewa mpana na wa kina miongoni mwa wanajamiii na kuweza kuchukua hatua kulingana na mlichojifunza ili kuleta mabadiliko chanya.

Tunawahimiza kuwa katika vikundi na kujadili maudhui haya kwa namna ambayo itawafaa zaidi.

Watch HerStory video compilation

VIDEO: Simulizi za Ujasiri, Uthubutu, na Mafanikio

Makala ya video yenye simulizi za Madiwani wanawake watatu kutoka mkoa wa Morogoro. Video hii ipo kwa Kiswahili.

AUDIO: Simulizi za Ujasiri, Uthubutu,na Mafanikio

Makala ya Sauti yenye Simulizi za Madiwani wanawake watatu kutoka mkoa wa Morogoroo. Makala hii ipo kwa lugha ya Kiswahili.
Drama video image

MAIGIZO YA VIDEO

Maigizo ya video matatu kuhusu ushiriki wa wanawake katika uongozi.
Scroll to Top